YOUNG AFRICANS yaigalagaza AZAM FC kwa kichapo kinono kule Zanzibar , Amani complex
Wachezaji waliohusika katika kufunga magoli hayo ya YOUNG AFRICANS;
1. IBRA BACCA, aliitanguliza YANGA kwa kuifungia goli la kwanza dakiki ya 41', pasi iliyopigwa na mshambuliaji nyota wa Yanga prince Dube.
2. LAURINDO AURELIO (DEPU) Raia wa Angola , aliifungia Yanga goli la pili dakiki ya 73' baada ya mchezaji Pacome Zouzoua kufanyiwa fouls na mlinzi wa AZAM FC na Mwamuzi kuamuru ipigwe mkwaju wa penalti.
3. PACOME ZOUZOUA Raia wa ivory coast, aliifungia Yanga goli la tatu dakika ya 81' mpira uliokuwa kwa kubabatiza ukamkuta kiungo mshambuliaji huyo na kuifanya timu yake kuibuka na ushind wa 3 kwa 0.
YANGA imesalia kileleni kwa point 69 baada ya mazunguko 28 wa NBC premier league (LIGI KUU) kukamilika leo huku wakiwa wamewaacha wapinzani wao wa jadi SIMBA SC kwa alama ya point 2,
Mpaka sasa Yanga imejiweka sehemu nzuri ikiwa imebakisha mechi mbili kutamatika kwa mashindano ya LIGI KUU TANZANIA 🇹🇿 (NBC premier league) mwaka 2026, yanga kama wataendelea kwa ushindi wanaweza wakabeba ubingwa wa LIGI KUU msimu huu 2026
Je unahisi mechi zilobaki kwa Yanga hazitamutia ugumu katika kuutaka ubingwa wa NBC premier league au ataachia ubingwa shusha comment yako hapo chini👇👇👇.

Comments
Post a Comment
Maoni yako ni muhimu kwetu! Unafikiri nini kuhusu mchezo au tetesi hii ya leo? Shusha mchango wako hapa chini. Kumbuka: Lugha ya staha na heshima kwa wadau wote wa soka inazingatiwa.