🏟🎯SIMBA IPO KWENYE MAWINDO MAKALI YA KUMUNASA KIUNGO MSHAMBULIAJI RAIA WA NIGERIA🚨, IBRAHEEM JABAAR ⚽️
Klabu ya wekundu wa msimbazi SIMBA SC wanaoneka kudhamiria kuboresha katika safu ya kiungo mshambuliaji. Tetesi za ndani za michezo zinaeleze kuwa simba sc wameingia vitani kuwania saini ya mchezaji Raia wa Nigeria🇳🇬, IBRAHEEM JABAAR aliyekuwa ikiitumikia klabu ya stellenbosch Fc ya nchini Africa kusini.
Tetesi hizi zimepamba moto baada ya klabu ya stellenbosch kutangaza kuachana na mchezaji huyo baada ya kumaliza mkataba nae na kuwa mchezaji huru, ambapo ibraheem jabaar ameitumikia timu hiyo kwa mda wa misimu mitano iliyopelekea kutwaa baadhi ya tuzo.
Rekodi za ibraheem jabaar akiwa kwenye timu ya stellenbosch
1. Ameitumikia stellenbosch Fc kwa mda wa misimu mitano kuanzia February 2021 hadi June 2026
2.Amecheza mashindano ya kimataifa Caf confederation cup
3. Amecheza michezo 140 na kushinda tuzo ya mchezaji kijana kucheza michezo mingi kwenye timu hiyo
Mambo yanayopelekea kumfanya IBRAHEEM JABAAR kuwa mchezaji bora wa kipekee;
1. Mguu wake wa kushoto, jabaar anatumia silaha yake hiyo kwa kutengeneza pasi za mwisho, kutengeneza nafasi za magoli na kufunga pia.
2.Udhoefu wa soka, jabaar amecheze mashindano ya ushindani huko Africa kusini kwa misimu kalibia mitano na kuonesha ukomavu wa soka.
3. Mbinu yake ya uchezaji, jabaar ni mchezaji wa Kisasa na umri wake unaruhusu kufanya mambo makubwa uwanjani, anauwezo wa kuipatia timu yake ushindi.
SIMBA SC, Suala la viungo wabunifu limekuwa likiwapasua kichwa mashabiki wa Simba kwa muda mrefu. Kuja kwa mchezaji mwenye wasifu kama ya Jabaar kunaweza kuongeza nguvu ya ushindani na kuwapa mashabiki burudani ya soka la pasi fupi na la haraka ambalo klabu hiyo inasifika nalo.
Huku dirisha la usajili likiwa bado linaendelea, macho yote ya wapenzi wa soka nchini yameelekezwa Msimbazi kuona kama dili hili litakamilika rasmi.
Je wewe kama mashabiki damu damu wa weknudu wa msimbizi simba sc unahisi usajili huu utafanikiwa na jabaar ataleta matunda kwenye timu ya simba sc,? Shusha comment yako hapo chini 👇 👇👇
#SimbaSC #NguvuMoja #WekunduWaMsimbazi #TetesiZaUsajili #UsajiliTanzania #SokaLaBongo #HabariZaMichezo #LigiKuuYaNBC#SimbaKwanza #SimbaDay #SimbaTamuu #SimbaApp #Wanasimba #SimbaLeo

Comments
Post a Comment
Maoni yako ni muhimu kwetu! Unafikiri nini kuhusu mchezo au tetesi hii ya leo? Shusha mchango wako hapa chini. Kumbuka: Lugha ya staha na heshima kwa wadau wote wa soka inazingatiwa.