KIMENUKA MIXED ZONE! CRISTIANO RONALDO AZUA GUMZO BAADA YA KUULIZWA KUHUSU KUKUTANA NA ARGENTINA YA MESSI.
Masaa machache yaliyopita yamekuwa ya mkanganyiko wa sintofahamu kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, baada ya nahodha wa Ureno, Cristiano Ronaldo, kuonyesha pande mbili alipoulizwa kuhusiana na mpinzani wake wa mda mrefu Lionel Messi, kwenye mashindano ya FIFAWORLDCUP🌎
UPANDE WA KWANZA: Ronaldo kukwepa swali kuhusu Messi,'
Ronaldo alipokuwa kwenye mahojiano ya (Mixed Zone), Mwandishi mmoja alijaribu kumuuliza swali kuwa ; JANA MESSI..' kabla hajamaliza kuuliza swali Cristiano Ronaldo nahodha huyo wa Ureno aliwahi na kumkatisha kwa kusema "NEXT QUESTION" (swali linalofuata).
Nahodha huyo wa Ureno hakutaka kuzungumzia ulinganisho uliopo dhida ya yeye na messi, ulinganisho huo usiokuwa na tija, Ronaldo alionekana akili yake yote kajiandaa kwaajili ya kuifikisha juu timu yake na matarajio yake ni kuhakikisha anabeba FIFA WORLD CUP🌎 2026
UPANDE WA PILI: Ronaldo afunguka kuhusu mpinzani wake Messi
Cristiano Ronaldo alikaa akaturia baada ya hapo alisimama kwenye mahojiano mengine tena, kwenye maikrofoni za waandishi wa habari kwa ajili ya mahojiano rasmi ya baada ya mchezo, mara hii alijibu akiwa ametabasamu na kusema "Kucheza dhidi ya Lionel Messi kwenye Kombe la Dunia? Swali hili halina maana sana kwa sasa... lakini sawa, nitajibu: utakuwa ni mchezo wa kiwango cha juu zaidi"
Je, ni kweli star🌟 huyo wa mda wote, Cristiano Ronaldo anakuwa na hofu akitajwa mpinzani wake nahodha wa Argentina? Shusha comment yako hapo chini 👇👇👇

Comments
Post a Comment
Maoni yako ni muhimu kwetu! Unafikiri nini kuhusu mchezo au tetesi hii ya leo? Shusha mchango wako hapa chini. Kumbuka: Lugha ya staha na heshima kwa wadau wote wa soka inazingatiwa.