HISTORIA YA ALPHONCE MSANGA (MABULA) YA SOKA: Kutoka kwenye maisha ya mtaani hadi kuwa mchezaji bora wa kimataifa
ALPHONCE MSANGA (MABULA), ni miongono mwa viungo wanaotajwa kuwa na viwango wa kimataifa na wenye umri mdogo nchi Tanzania kw sasa.
Maisha ya Awali na Soka la mtaani;
Mabula alizaliwa na kukulia Tanzania kama walivyo vijana wengine, Alijiunga na soka la vijana wa mtaani akiwa na umri mdogo sana, alianza kucheza kiungo mkabaji, uwezo wake wa soka, utulivu, upigaji pasi sahihi na ukakamavu vilianza kuonekana kwenye mashindano ngazi ya shule na mitaani.
Maisha na malezi ya Spartan academy (Spartan Boys);
Mabula alijiunga na kituo cha mpira cha kulea na kukuza vipaji vya vijana kilichopo Dar Es Salaam. Hapa ndipo alipoanza kupata mafunzo na maisha ya soka, Spartan academy ikiwa na viwango bora vya makocha vilimpelekea Mabula kiwango chake kupanda kwa haraka na kuwa mchezaji mwenye kuaminika, hapa ndo alifundishwa namna ya kuusoma mchezo, namna ya kukaa kwenye eneo, namna ya ukabaji, na namna ya kujiamini akiwa uwanjani.
Timu ya vijana ya soka Tanzania;
Kwa kiwango alichokuwa nacho Mabula kwenye kituo hicho cha Spartan Boys Academy, Makocha wa timu ndogo ya Tanzania walimuchukua na kumuunga na wachezaji wenzake, Mabula alijiunga na timu ya Taifa ya Tanzania ya umri chini ya miaka 17 (under 17) Serengeti Boys, kwenye umri huu alionesha mkakamavu na mwenye kiwango cha hali ya juu kwenye mashindano ya AFCON na CECAFA ya vijana.
Safari ya maisha ya kulipwa ulaya kwenye timu ya Şamaxı FK (Azerbaijan);
Mabula alijiunga na timu ya Şamaxı FK ya Azerbaijan. Hapa ndo safari ya maisha ya kulipwa yalianza, wakala wa timu ya hiyo ya ulaya walivutiwa na kiwango cha Mabula na kumsajili akiwa na umri mdogo kwenda kuitumikia timu hiyo. Tofauti na wachezaji wengine wengi wa Tanzania ambao mpaka wapite Ligi Kuu NBC ndo wanapata na nafasi za kwenda kutumikia timu za ulaya, lakini kwa Mabula yeye alipata bahati ya moja kwa moja kutoka Spartan academy na kupita Serengeti Boys baada ya hapo na kuchukuliwa timu ya ulaya.
Uzoefua wa ligi ya ulaya;
Mabula alianza kujifunza mbinu nyingi na kuona utofauti wa soka la bongo na Ulaya ambapo akiwa ulaya alionesha kiwango kizuri sana. Kwenye mashindano yaliyoshikwa na timu yake alionesha utulivu wa hali ya juu, uwezo wa hali ya juu na utimamu wa soka mpaka makataba wake ulipotamatika rasmi 30 Juni, 2026.
Timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars);
Kwa kiwango kikubwa alichokionesha akiwa Şamaxı FK ya Azerbaijan, ulaya benchi la ufundi la timu ya Taifa lilimuita kuja kulitumikia Taifa lake, alionesha umahili na kiwango kikubwa kwenye mashindano ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON).
Sifa zake kuu Alphonce Masanga (Mabula);
•Nguvu na ukabaji; ana uwezo wa kupokonya(kunyang'anya) mipira bila kufanya madhambi yoyote yale.
•Utimamu wa akili; ana utulivu wa hali ya juu hapaniki wala hateteleki akiwa na mpira.
•Pasi; ana uwezo wa kupiga mipira mirefu na mifupi wa ufundi wa hali ya juu bila kukosea.

Comments
Post a Comment
Maoni yako ni muhimu kwetu! Unafikiri nini kuhusu mchezo au tetesi hii ya leo? Shusha mchango wako hapa chini. Kumbuka: Lugha ya staha na heshima kwa wadau wote wa soka inazingatiwa.