UJIO MPYA WA SHEREHE YA KILELE CHA WIKI YA MWANANCHI (Yanga day).

Mashabiki wa Yanga sc, wanajangwani kaeni mkao wa kula maana msimu huu yanga sc imekuja kwa vingine tofauti na miaka mingine akisema Rais wa klabu  yanga sc,Injinia Hersi Said  "Kuelekea katika kilele cha mwananchi Yanga day,  maandalizi ya sherehe hiyo teyari yameshakamilika kila kitu kwa idara zote". 


Injinia Hersi Said alipokuwa kwenye mji wa Katoro-Geita kupitia taarifa ya habari ya azam Tv alizungumza maneno hayo siku ya ijumaa tarehe 24 mwezi huu na kuutaja mji wa Katoro ndiyo utakaotumika kwaajili ya wiki ya mwananchi na kufafanua ratiba na muongozo watakao kuwa nao Kuelekea yanga day;

    1. Injinia Hersi Said, alitangaza mwisho wa                mwezi huu kutakuwa na uzinduzi wa jezi              zitakazotumika msimu wa 2026/2027.
    2. Mkutano mkuu wa mwaka wa yanga sc                  utakaofanyika mwezi wa nane tarehe 2.                 (agosti 2, 2026).
   3. Mwanza, matukio maalumu na uzinduzi wa         yanga sc Kuelekea Yanga day utahamia                   kwenye Jiji hilo kati ya tarehe 3 au 4 mwezi.         wa nane(agosti).
   4. Tarehe 9 agosti, 2026 hii siku ndiyo                           itakakayokuwa hitimisho la sherehe za                   Yanga day, utambulisho wa wachezaji                     waliosajiliwa(maingizo mapya) na                           waliokuwepo, sherehe hiyo itafanyika                     kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na         kutakuwa na mechi ya kirafiki. 

 Malengo ya klabu ya Yanga sc msimu huu;

Maandalizi ya kuelekea msimu huu wa Ligi Kuu NBC, teyari Yanga sc washaanza kujiandaa na pre-season. Yanga sc msimu huu wanatarajia kuwa mabingwa tena kwa mara nyingine msimu huu 2026/2027, na nguvu zao nyingi hasa wamezielekezea kwenye mashindano makubwa ya ushindani  hasa mashindano ya kimataifa, Ligi ya mabingwa Afrika (Caf Champions League).

Pia Yanga sc wamepania kubeba ndoo za ligi za ndani kama kombe la shirikisho (CRDB BANK Federation Cup, kombe la muungano pamoja na ngao ya jamii.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA ALPHONCE MSANGA (MABULA) YA SOKA: Kutoka kwenye maisha ya mtaani hadi kuwa mchezaji bora wa kimataifa

Wachezaji bora kwenye ligi kuu ya NBC Premier League

Wasifu wa Albert Kangwanda Jr: Nyota Mpya wa Kimataifa Anayetamba Ndani ya Kikosi cha Yanga SC

RIPOTI KUTOKA KAMBINI: Uchambuzi wa Kikosi cha Taifa Stars na Silaha Mpya Kuelekea AFCON 2027

Fabrizio Romano Aitambulisha Yanga Duniani, Bodi ya Ligi Yaibeba Simba SC!

Rungu la TPLB: Maafisa wa Singida Black Stars Watandikwa Faini ya Tsh Milioni 20!

Mtanange wa Ligi Kuu ya NBC: Uchambuzi wa Kina wa Mechi za Kukata na Shoka Kesho

Mwelekeo wa Ligi Kuu ya NBC: Rejesho la Aziz Ki, Changamoto ya Majeraha Simba SC na Shinikizo Ndani ya Azam FC

WASIFU KAMILI: Fahamu Nguvu na Udhaifu wa Gaborone United, Wapinzani wa Yanga SC Ligi ya Mabingwa Afrika!

Ratiba Kamili na Utabiri wa Kimbinu wa Michezo ya Ufunguzi Ligi Kuu ya NBC Wikiendi Hii.