Rungu la TPLB: Maafisa wa Singida Black Stars Watandikwa Faini ya Tsh Milioni 20!
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeshusha rungu zito kwa viongozi wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Singida Black Stars, kufuatia mfululizo wa matukio ya utovu wa nidhamu na ukiukwaji wa maadili ya mchezo wa soka nchini. Katika kikao chake cha hivi karibuni, kamati hiyo imewatoza faini ya jumla ya Shilingi Milioni Ishirini (Tsh 20,000,000) maafisa wawili wa klabu hiyo, Hussein Massanza na Pablo Almasi, baada ya kupatikana na makosa ya kashfa, matusi, na kuibeza teknolojia mpya ya usaidizi wa waamuzi kwa video (FVS). Hussein Massanza Atandikwa Faini ya Milioni 10 Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Singida Black Stars, Hussein Massanza, amekumbana na rungu hilo baada ya kutumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kutoa lugha ya matusi na shutuma nzito dhidi ya waamuzi. Hatua hii ilikuja mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Singida Black Stars na Simba SC, ambapo Singida walipoteza kwa mabao 2-...