Posts

Showing posts from June, 2026

KIMENUKA: Siri ya Usajili wa Simba na Yanga Yavuja, Vita ya Kuwania Saini ya Staa wa Azam FC Yatafuta Mchawi!

Image
Msukosuko wa usajili kwenye Ligi Kuu ya NBC umezidi kushika kasi huku klabu kubwa za Simba SC , Young Africans (Yanga) , na Azam FC zikitengeneza vikosi vya maangamizi. Habari za ndani kabisa zinasema kuwa klabu ya Simba imeweka dau nono mezani kujaribu kunasa saini ya mchezaji tegemeo, huku Yanga nao wakipanga mapinduzi makubwa ili kulinda ubingwa wao. Mashabiki wa soka kote nchini wamebaki na maswali mengi kuhusu hatma ya nyota hawa huku presha kubwa ikizidi kupanda kuelekea michezo inayofuata ya ligi.  🚨 NYONGEZA MUHIMU : Kama unataka kusoma mkataba kamili, dau la usajili, na kuona siri zote zilizofichwa kuhusu mchezaji huyu kwenye simu yako: Wataalamu wa soka wanasema usajili wa msimu huu utakuwa na ushindani mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya soka la Tanzania. Endelea kufuatilia blogu yetu kwa habari zaidi za ukweli na uhakika kila saa!

VIWANJA NANE KUWAKA MOTO: Raundi ya 29 ya NBC Premier League Kupigwa Leo kwa Muda Mmoja.

Image
Msisimko wa Ligi Kuu ya NBC unafikia kilele chake leo Jumamosi ya tarehe 27 Juni, ambapo timu zote 16 zitashuka dimbani kucheza michezo nane ya raundi ya 29 kwa muda mmoja, saa 10:00 jioni. Hatua hii ya Bodi ya Ligi imelenga kuongeza ushindani wa haki na kuzuia mianya ya upangaji wa matokeo, huku presha kubwa ikiwa pande zote mbili; zile zinazowania ubingwa na zinazopambana kushuka daraja. Macho ya mashabiki wengi yatakuwa jijini Dar es Salaam ambapo Young Africans watakuwa wenyeji wa TRA United kwenye uwanja wa KMC Complex, huku majirani zao Simba SC wakicheza dhidi ya Singida Black Stars kwenye dimba la Meja Jenerali Isamuhyo lililopo Mbweni. Vita nyingine kali itakuwa mkoani Tanga ambapo Azam FC watakuwa wageni wa Coastal Union , mchezo utakaotoa mwelekeo wa nani atakayeshika nafasi za juu za msimamo msimu huu.

RASMI: Simba SC Yakamilisha Usajili wa Winga Machachari Bakari Msimu Kutoka Coastal Union

Image
Baada ya mvutano wa muda mrefu chini kwachini,hatimaye dili limekamilika ambapo Simba SC imefanikiwa kunasa saini ya winga wa kulia wa Coastal Union, Bakari Msimu (18). Kinda huyo machachari amesaini kandarasi ya miaka mitatu kuitumikia miamba hiyo ya Msimbazi baada ya kugoma kusaini mkataba mpya na klabu yake ya zamani ya Coastal Union iliyokuwa na mpango wa kumfunga mkataba ili kumfanya bidhaa ya biashara. Usajili huu umepishwa moja kwa moja na kocha mkuu Steve Baker , ambaye alivutiwa na kasi kubwa, uwezo wa kupiga chenga, na njaa ya mafanikio aliyonayo kijana huyo. Mashabiki wameupokea usajili huu kwa matumaini makubwa wakiamini Msimu anaenda kuwa nguzo mpya ya ushambuliaji wa pembeni klabuni hapo. Mipango ya Muda Mrefu na Changamoto Inayomkabili Msimu Uamuzi wa Simba SC kuwekeza kwa Bakari Msimu unaonekana kama mkakati wa muda mrefu wa klabu hiyo kuanza kujenga kikosi chenye vijana wadogo (youth project). Katika misimu ya karibuni, Wekundu wa Msimbazi wamekuwa wakikosolewa ...

DAU NONO: Azam FC Yamfunga Mkataba Mrefu Winga Iddy Nado Kuzima 'Mind Games'

Image
Klabu ya soka ya Azam FC "Wanalambalamba" wameamua kuingia mfukoni na kuzima rasmi tetesi zote zilizokuwa zikimuhusisha mshambuliaji wao machachari, Iddy Suleiman 'Nado ', na vilabu vingine. Uongozi wa Azam FC chini ya maelekezo ya Kocha Mkuu Florent Ibenge , umekamilisha taratibu za kumpa winga huyo mkataba mpya na mnono wa kuendelea kusalia klabuni hapo. Kocha Ibenge amesisitiza kuwa katika mikakati yake mipya, hakuna mchezaji yeyote muhimu atakayeruhusiwa kuondoka kwa sasa. Hatua hii inatajwa kuzima mbinu za kisaikolojia (mind games) zilizokuwa zikitumiwa na wapinzani wao wakati wa kuelekea mechi muhimu za CRDB Bank Federation Cup.

VITA YA VILABU: Yanga na Azam FC Waingia Kwenye Vita Kali Kunasa Saini ya Chobwedo

Image
Soko la usajili limezidi kuchafuka nchini baada ya klabu za Yanga SC na Azam FC kuingia vitani vikali kuwania saini ya kiungo tegemeo wa TRA United , Ramadhani Chobwedo . Chobwedo amekuwa lulu sokoni kutokana na uwezo wake mkubwa aliouonesha msimu huu, jambo linalomfanya kila tajiri wa soka kutaka kuweka mzigo mezani. Wakati Azam wakijinasibu kwa dau nono, Yanga   wanatumia ushawishi wa kushiriki michuano mikubwa kama chambo cha kumnasa kiungo huyo. Mashabiki wanasubiri kuona ni wapi mchezaji huyo atatua huku akitajwa pia kuwa kwenye rada za Simba Sc.

HATMA YA MUTALE: Klabu ya Al Adalah Yamrudisha Simba SC, Mabingwa wa Msimbazi Wagoma Kumpokea.

Image
Wakati dirisha la usajili likizidi kushika kasi nchini, mustakabali wa kiungo mshambuliaji raia wa Zambia, Joshua Mutale 'Budo' , umekuwa gumzo kubwa baada ya kujikuta njia panda kufuatia hatua ya klabu ya Al Adalah Club ya Saudi Arabia kugoma kumsajili mazima. Mutale alikuwa akicheza nchini Saudi Arabia kwa mkopo wa miezi sita uliomshuhudia akicheza mechi 12 na kuifungia klabu hiyo mabao mawili. Al Adalah Wagoma Kumnunua Jumla Taarifa za uhakika kutoka Mashariki ya Kati zinasema kuwa viongozi wa Al Adalah wamewaandikia rasmi viongozi wa Simba SC kuwajulisha kuwa hawana mpango wa kuamsha kipengele cha mkataba kinachoruhusu kumnunua kiungo huyo kwa mkataba wa kudumu. Mkataba wake wa mkopo unatarajiwa kufikia ukomo rasmi ifikapo Juni 30, 2026 . Simba SC Nao Wafunga Milango Msimbazi Licha ya kuwa Joshua Mutale bado ana mkataba wa mwaka mmoja uliobaki na miamba hiyo ya Msimbazi (hadi Juni 30, 2027), taarifa za ndani zinasema kuwa benchi la ufundi la Simba halina mpango wa kumjumui...

RASMI: Ismail Mgunda Atua Simba SC, Kusaini Kandarasi ya Miaka Miwili

Image
Klabu ya Simba inaendelea kutikisa soko la usajili nchini baada ya kukamilisha taratibu zote za kumnasa mshambuliaji wa kati, Ismail Mohamed Mgunda , akitokea kikosi cha Mashujaa FC ya mkoani Kigoma. Usajili huu unalenga kuongeza nguvu, uzoefu, na makali mapya kwenye safu ya ushambuliaji ya Wekundu wa Msimbazi kuelekea msimu mpya wa mashindano. Maelezo Kuhusu Mkataba Wake; Habari za uhakika kutoka ndani ya klabu zinasema kuwa Mgunda amemwaga wino wa kuitumikia miamba hiyo ya Msimbazi kwa mkataba wa miaka miwili. Mazungumzo kati ya pande zote mbili yalikwenda vizuri, na pande zote ziliridhia masharti ya usajili huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu. Uzoefu na Changamoto za Majeraha; Ismail Mgunda, mwenye umri wa miaka 30, si jina geni kwenye masikio ya wapenzi wa soka la bongo. Amekuwa mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kupambana na walinzi na kulinda mpira anapokuwa eneo la hatari. Licha ya kwamba msimu uliopita alikabiliwa na changamoto kadhaa za majeraha zilizomfanya akose baadhi ya mechi a...

🔥 RATIBA YA LALA SALAMA NBC PREMIER LEAGUE: MECHI ZA MWISHO ZAACHA MASWALI MAZITO! 🔥

Image
Msimu wa Ligi Kuu ya NBC 2025/2026 unafikia tamati wiki hii, na bodi ya ligi imeshapanga ratiba ya mechi za mwisho zitakazochezwa kati ya kesho kutwa tarehe 28 Juni na tarehe 30 Juni, 2026. Msimu huu umekuwa na ushindani mkubwa sana kuanzia nafasi za juu za ubingwa na uwakilishi wa kimataifa, hadi timu zinazopambana chini kujinusuru kushuka daraja. Kuelekea michezo hii ya mwisho, presha imepanda kwa wachezaji, makocha, na mashabiki wa soka nchini Tanzania kwa sababu kila pointi moja sasa hivi inaamua hatuzi ya klabu kwa msimu ujao .   Je, ni timu gani zitafanikiwa kukaba nafasi zao na zipi zitaaga ligi kuu? Endelea kufuatilia blogu yetu kwa matokeo ya moja kwa moja pindi mechi hizo zitakapopigwa!

Mapinduzi Makubwa Yanga SC: Vyuma Vya Kimataifa Kutua Jangwani, Kusafisha Kikosi kuelekea msimu ujao, 2026/27.

Image
Uongozi wa klabu ya Yanga SC umeingia rasmi kwenye mipango mizito ya kusuka upya kikosi chao kuelekea msimu ujao. Safari hii, mabingwa hao wa kihistoria hawatazami tu kutawala soka la ndani kupitia Ligi Kuu ya NBC, bali macho yao yote yapo kwenye anga la kimataifa. Lengo kuu la miamba hiyo ya Jangwani ni kuhakikisha wanafika hatua ya nusu fainali au fainali ya Klabu Bingwa Afrika (CAF Champions League). Ili kufanikisha azma hiyo, benchi la ufundi la Yanga limeweka wazi maeneo matatu yanayohitaji maboresho ya haraka ili kuongeza makali ya timu: Safu ya ushambuliaji ya kati kwa ajili ya mabao. Kiungo mbunifu atakayechezesha timu na kutengeneza nafasi. Beki wa pembeni mwenye kasi na uwezo wa kushambulia. Sura Mpya Zenye Wasifu wa Kimataifa Katika kukidhi matakwa hayo, Yanga inaripotiwa kukamilisha mazungumzo ya awali na mshambuliaji hatari kutoka ukanda wa Afrika Kaskazini. Nyota huyu anakuja maalum kwa ajili ya kutatua tatizo la ufungaji kwenye mechi kubwa za kimataifa ambalo lilijito...

YANGA KUIKABILI SIMBA SC KWENYE FAINALI YA CRDB BANK FEDERATION CUP DHIDI YA AZAM FC

Image
Mashabiki wa soka nchini wajiandae kwa burudani ya aina yake visiwani Zanzibar, Kauli ya hivi punde ya Meneja wa Habari wa Yanga, ALI KAMWE , imethibitisha kuwa fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB kati ya Simba SC na Azam FC haitakuwa ya kawaida hata kidogo.  Baada ya yanga kukwama kwenye nusu  fainali ya CRDB,  ali kamwe amesimama na kuzungumza kuwa "sisi yanga tutaisapoti azam fc kwenye fainali ya CRDB huko ZANZIBAR PEMBA kwenye uwanja  wa Gombani,  kuelekea fainali hiyo mashabiki wa yanga wataungana na azam fc kuhakikisha azam fc inabeba kombe. Utani wa jadi bado unazidi kukua siku hadi siku na sasa upinza huu umegeukia kwa mashabiki, tunategemea kuja kutazama mchezo mzuri na wenye burudani ukiwa na pande mbili za ushindani , huku timu ya azam Fc vs simba sc  na kw mashabiki ni yanga wakiungana na azam fc  vs mashabiki wa Simba SC.  Hali hii kwa timu ya simba inapelekea kusongwa na seheme kubwa ya upinzani kwenye fainali, ikiwata simba kuj...

🏟🎯SIMBA IPO KWENYE MAWINDO MAKALI YA KUMUNASA KIUNGO MSHAMBULIAJI RAIA WA NIGERIA🚨, IBRAHEEM JABAAR ⚽️

Image
Klabu ya wekundu wa msimbazi SIMBA SC wanaoneka kudhamiria kuboresha katika safu ya kiungo mshambuliaji. Tetesi za ndani za michezo zinaeleze kuwa simba sc wameingia vitani kuwania saini ya mchezaji Raia wa Nigeria🇳🇬, IBRAHEEM JABAAR aliyekuwa ikiitumikia klabu ya stellenbosch Fc ya nchini Africa kusini . Tetesi  hizi zimepamba moto baada ya klabu ya stellenbosch kutangaza kuachana na mchezaji huyo baada ya kumaliza mkataba nae na kuwa mchezaji huru, ambapo ibraheem jabaar ameitumikia timu hiyo kwa mda wa misimu mitano iliyopelekea kutwaa baadhi ya tuzo. Rekodi za ibraheem jabaar akiwa kwenye timu ya stellenbosch   1. Ameitumikia stellenbosch Fc kwa mda wa misimu mitano kuanzia February 2021 hadi June 2026 2.Amecheza mashindano ya kimataifa Caf confederation cup 3. Amecheza michezo 140 na kushinda tuzo ya mchezaji kijana kucheza michezo mingi kwenye timu hiyo Mambo yanayopelekea kumfanya IBRAHEEM JABAAR kuwa mchezaji bora wa kipekee ; 1. Mguu wake wa kushoto , jabaar anat...

YOUNG AFRICANS yaigalagaza AZAM FC kwa kichapo kinono kule Zanzibar , Amani complex

Image
Zanzibar imeshuhudia mchezo mzuri uliomalizaka katika viwanja vya AMANI COMPLEX , Zanzibar ikiwakutanisha magwiji wa soko YOUNG AFRICANS dhidi ya AZAM FC ambao mchezo umetamatika kwa YOUNG AFRICANS kuibuka na ushindi mnono wa 3 kwa 0, Wachezaji waliohusika katika kufunga magoli hayo ya YOUNG AFRICANS ;  1. IBRA BACCA , aliitanguliza YANGA kwa kuifungia goli la kwanza dakiki ya 41', pasi iliyopigwa na mshambuliaji nyota wa Yanga prince Dube. 2. LAURINDO AURELIO (DEPU ) Raia wa Angola , aliifungia Yanga goli la pili  dakiki ya 73' baada ya mchezaji Pacome Zouzoua kufanyiwa  fouls  na mlinzi wa AZAM FC na Mwamuzi kuamuru ipigwe mkwaju wa penalti. 3. PACOME ZOUZOUA Raia wa ivory coast, aliifungia Yanga goli la tatu dakika ya 81' mpira uliokuwa kwa kubabatiza ukamkuta kiungo mshambuliaji huyo na kuifanya timu yake kuibuka na ushind wa 3 kwa 0. YANGA imesalia kileleni  kwa point 69 baada ya  mazunguko 28 wa NBC premier league (LIGI KUU ) kukamilika leo hu...

YOUNG AFRICANS 1 vs 0 AZAM FC dakika ya 41

GOOOOOOOOOL🥅 IBRAHIM BACCA 1 VS 0 AZAM FC

KIMENUKA MIXED ZONE! CRISTIANO RONALDO AZUA GUMZO BAADA YA KUULIZWA KUHUSU KUKUTANA NA ARGENTINA YA MESSI.

Image
Masaa machache yaliyopita yamekuwa ya mkanganyiko wa sintofahamu  kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, baada ya nahodha wa Ureno , Cristiano Ronaldo , kuonyesha pande mbili alipoulizwa kuhusiana na mpinzani wake wa mda mrefu Lionel Messi , kwenye mashindano ya FIFAWORLDCUP🌎 UPANDE WA KWANZA : Ronaldo kukwepa swali kuhusu Messi,' Ronaldo alipokuwa kwenye mahojiano ya (Mixed Zone), Mwandishi mmoja alijaribu kumuuliza swali kuwa ; JANA MESSI ..' kabla hajamaliza kuuliza swali Cristiano Ronaldo nahodha huyo wa Ureno aliwahi na kumkatisha kwa kusema "NEXT QUESTION" (swali linalofuata). Nahodha huyo wa Ureno hakutaka kuzungumzia ulinganisho uliopo dhida ya yeye na messi, ulinganisho huo usiokuwa na tija, Ronaldo alionekana akili yake yote kajiandaa kwaajili ya kuifikisha juu timu yake na matarajio yake ni kuhakikisha anabeba FIFA WORLD CUP🌎 2026 UPANDE WA PILI : Ronaldo afunguka kuhusu mpinzani wake Messi Cristiano Ronaldo alikaa akaturia baada ya hapo alisimama kwenye...

Vita Mpya ya Kisheria na Maneno: Julián Álvarez Achochea Mgogoro Mzito Kati ya Atlético Madrid na Barcelona.

Image
Ulimwengu wa soka umezizima kufuatia mzozo mpya na mkubwa wa usajili unaosikika nchini UHISPANIA , safari hii ukihusisha klabu kubwa mbili; Atlético Madrid na FC Barcelona . Kiini cha dhoruba hii si mwingine bali ni mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina , Julián Álvarez . Sakata hili lililochukua sura mpya ghafla, limehama kutoka kwenye tetesi za kawaida za usajili na sasa linaelekea kwenye vyombo vya sheria vya soka vya kimataifa. Ndoto ya Álvarez na Tamko la Kulazimisha Uhamisho Kila kitu kilianza pale mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City alipovunja ukimya na kuweka wazi nia yake ya kutaka kufungashiwa virago ndani ya jiji la Madrid. Álvarez alinukuliwa akisema kuwa "uamuzi wangu bora zaidi kwa sasa ni kupata uhamisho ili niweze kutimiza ndoto yake." Inafahamika kuwa nyota huyo ameshafanya mazungumzo ya faragha na uongozi wa Los Colchoneros na kuwajuza kuwa akili yake yote ipo nje ya klabu hiyo. Ripoti za ndani zinasema kuwa mchezaji huyo tayari ameshafikia mak...

LIONEL MESSI afanya Maajabu Tena! Avunja Rekodi ya Dunia Kwenye Mechi ya Leo na Kuongoza Chati za FIFA

💯Mashabiki wamezidi tena kujionea leo Messi kuandika historia mpya kwenye ulimwengu wa soka leo baada ya kuiongoza Argentina kupata ushindi mnono wa magoli 2-0 dhidi ya Austria katika hatua ya makundi ya Kombe la Dunia 2026. Katika mechi hiyo kali iliyopigwa leo Juni 22, 2026, nahodha huyo wa Argentina amefunga mabao yote mawili na kuihakikishia timu yake nafasi ya kutinga hatua ya 32 bora. ⚽️Messi baada ya kukosa penalti mwanzoni mwa mchezo, alirejea kwa kishindo na kufunga magoli mawili, goli la kwanza dakiki ya 38 na goli la pili dakika ya 90+4 nakuipatia timu yake ushindi🏅 mnono.  Messi amevunja record ya mastar wa kubwa waliopita kwenye KOMBE LA DUNIA baada ya kufunga magoli leo mawili nakufikisha magoli 18 toka yameanzishwa mashindano ya KOMBE LA DUNIA . Takwimu za Messi baada ya mchezo huu kumalizika kwa Sasa Kufuatia kiwango hicho safi alichoonyesha leo na hat-trick aliyopiga kwenye mechi iliyopita dhidi ya Algeria, nafasi za Lionel Messi zimepanda kwa kasi, Lionel...

KYLIAN MBAPPÉ AFUNGUKA: "Wanaosema Ronaldo Hana Kipaji na Messi Hafanyi Kazi Ngumu Hawajui Mpira"

Image
Mshambuliaji nyota wa kimataifa, Kylian Mbappé , amewatolea uvivu mashabiki na wachambuzi wa soka wanaolinganisha mafanikio ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kwa mtazamo hasi. Akijibu swali kwenye mahojiano maalum kuhusu nani bora kati yake, Erling Haaland, Harry Kane, na Lionel Messi, Mbappé aliamua kuweka wazi ukweli kuhusu magwiji hao wawili wa soka duniani. Mbappé amepinga vikali dhana ya muda mrefu inayodai kuwa Cristiano Ronaldo amefanikiwa kwa sababu ya kufanya kazi kwa juhudi tu bila kuwa na kipaji, na kwamba Messi anategemea kipaji pekee bila kufanya kazi ngumu. Kauli ya Mbappé :"Kama unaweza kuniangalia machoni na kuniambia kuwa Cristiano hana kipaji au Messi hajawahi kufanya kazi ngumu, basi wewe hujawahi kabisa kucheza mpira ( kuvaa viatu vya soka ) maishani mwako." 🇫🇷Mfaransa huyo alieleza kuwa ili mchezaji afike kiwango cha juu na kukaa hapo kwa miaka mingi kama walivyofanya Messi na Ronaldo , lazima uwe na mchanganyiko wa kipaji kikubwa sana pamoj...

🏆FAINALI IMEWIVA 🔥MOTO WA KICHAPO NI ULE ULE Azam Fc yatinga fainali ya CRDB BANK FEDERATION CUP kuivaa Simba Sc

Image
Nusu fainali ya CRDB BANK FEDERATION CUP   imetamatika kule Mwanza katika viwanja vya Ccm Kirumba baada ya AZAM FC   kuibuka na ushind wa goli 3 kwa 2 dhidi ya magwiji wa jangwani YOUNG AFRICANS .  AZAM FC   imetanguliza salamu kwa wekundu wa msimbazi wakisema kuwa kombe la CRDB BANK FEDERATION CUP 🏆, linaenda Chamazi. Je ni kweli kombe la CRDB BANK FEDERATION CUP litabaki kwa vijana wa Chamazi AZAM FC au litakwenda kwa wekundu wa msimbazi SIMBA SC ? Weka comment yako hapo chini 👇👇👇.

AZAM FC WA MOTO NUSU FAINALI YA CRDB BANK FEDERATION CUP

Image
🔥AZAM FC wapo teyari kila idara zote ukianza na benchi la ufundi, wachezaji kwa ujumla wote wamejiandaa kuhakikisha wanashinda🆙️ na kusonga mbele kuelekea fainali ya CRDB BANK FEDERATION CUP.  Azam Fc wamekuja idadi isiyopungua 45 kuonesha kuwa wanania na wanamalengo ya kuvuka hatua hiyo na kuelekea fainali.      Tumejiandaa, tupo tayari  na  tuna                                           hamu  na   yanga

Wachezaji bora kwenye ligi kuu ya NBC Premier League

Image
Ligi kuu Tanzania, NBC premier league mpaka sasa top 1-3 inashikiriwa na wachezaji hatari🔥, wenye utaaramu wa mpira⚽️, akili ya mpira, na ubora wa juu💯. 📊 Jedwali la Takwimu (Msimu wa 2025/2026)                                   Mchezaji. Feitoto               Timu.           Azam   Fc               Mabao.         14   Pasi za Goli (Assists) 7     Mchezaji     Allan Okello .               Timu          Young Africans .           Mabao.        11 .                                 Pasi za Goli (Assists))   7   Mchezaji  ...

NUSU FAINALI YA CRDB BANK FEDERATION CUP.

Image
MZIZIMA DERBY. Nusu fainali ya CRDB BANK FEDERATION CUP, ikiwakutanisha vijana wa baba mmoja na mama mmoja. Yaani hawa tunawazungumzia vinala wa soka ambao wote wanatoka sehemu moja, Dar es Salaam.                                                                                                     AZAM FC vs YOUNG AFRICANS , Yaani huku Feisal Salum "Feitoto" kule Allan Okello!. Je, nani atatangulizika karata yake fainali?                                                 Mwanza itasimama kwa muda siku ya kesho, tarehe 21 Juni 2026.  Muda saa 9:30 alasiri.

Burudani inarejea, MZIZIMA DERBY

Image
Ile mechi tuliyokuwa tukiisubiri kwa hamu sasa imewadia. Inawakutanisha wababe wa soka Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla. Hapa tunawazungumzia YOUNG AFRICANS wakiwakaribisha AZAM FC.  Mechi itapigwa kwenye uwanja wa KMC COMPLEX uliopo Kinondoni, Dar es Salaam.  Mchezo huu utapigwa siku ya Jumatano 24 June 2026, majira ya saa10:00 jioni.