KYLIAN MBAPPÉ AFUNGUKA: "Wanaosema Ronaldo Hana Kipaji na Messi Hafanyi Kazi Ngumu Hawajui Mpira"
Mshambuliaji nyota wa kimataifa, Kylian Mbappé, amewatolea uvivu mashabiki na wachambuzi wa soka wanaolinganisha mafanikio ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kwa mtazamo hasi.
<: 0.2="" 0="" 0px="" 100="" 4px="" 6px="" black="" box-shadow:="" color:="" display:="" font-family:="" gadget="" inline-block="" quot="" rgba="" rial="" scale="" transform:="" white="">
Akijibu swali kwenye mahojiano maalum kuhusu nani bora kati yake, Erling Haaland, Harry Kane, na Lionel Messi, Mbappé aliamua kuweka wazi ukweli kuhusu magwiji hao wawili wa soka duniani.
Mbappé amepinga vikali dhana ya muda mrefu inayodai kuwa Cristiano Ronaldo amefanikiwa kwa sababu ya kufanya kazi kwa juhudi tu bila kuwa na kipaji, na kwamba Messi anategemea kipaji pekee bila kufanya kazi ngumu.
Kauli ya Mbappé:"Kama unaweza kuniangalia machoni na kuniambia kuwa Cristiano hana kipaji au Messi hajawahi kufanya kazi ngumu, basi wewe hujawahi kabisa kucheza mpira (kuvaa viatu vya soka) maishani mwako."
🇫🇷Mfaransa huyo alieleza kuwa ili mchezaji afike kiwango cha juu na kukaa hapo kwa miaka mingi kama walivyofanya Messi na Ronaldo, lazima uwe na mchanganyiko wa kipaji kikubwa sana pamoja na nidhamu ya kufanya kazi kwa juhudi kila siku.
Je unakubaliana na kauli hii ya Kylian Mbappé kuhusu LIONEL MESSI na CRISTIANO RONALDO ? Weka maoni yako hapo chini👇👇


Comments
Post a Comment
Maoni yako ni muhimu kwetu! Unafikiri nini kuhusu mchezo au tetesi hii ya leo? Shusha mchango wako hapa chini. Kumbuka: Lugha ya staha na heshima kwa wadau wote wa soka inazingatiwa.