Vita Mpya ya Kisheria na Maneno: Julián Álvarez Achochea Mgogoro Mzito Kati ya Atlético Madrid na Barcelona.
Sakata hili lililochukua sura mpya ghafla, limehama kutoka kwenye tetesi za kawaida za usajili na sasa linaelekea kwenye vyombo vya sheria vya soka vya kimataifa.
Ndoto ya Álvarez na Tamko la Kulazimisha Uhamisho
Kila kitu kilianza pale mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City alipovunja ukimya na kuweka wazi nia yake ya kutaka kufungashiwa virago ndani ya jiji la Madrid. Álvarez alinukuliwa akisema kuwa "uamuzi wangu bora zaidi kwa sasa ni kupata uhamisho ili niweze kutimiza ndoto yake."
Inafahamika kuwa nyota huyo ameshafanya mazungumzo ya faragha na uongozi wa Los Colchoneros na kuwajuza kuwa akili yake yote ipo nje ya klabu hiyo. Ripoti za ndani zinasema kuwa mchezaji huyo tayari ameshafikia makubaliano ya kimaslahi na klabu ya Barcelona, hatua ambayo imewasha moto mkubwa nyuma ya pazia.
Atlético Madrid Yaamka, Yaelekea FIFA
Hasira za Atlético Madrid hazikuchukua muda mrefu kulipuka. Klabu hiyo inajiandaa kuwasilisha malalamiko rasmi mbele ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) dhidi ya FC Barcelona.
Atlético wanaituhumu Barça kwa kukiuka kanuni za usajili kwa kufanya mazungumzo ya siri na mchezaji ambaye bado ana mkataba wa muda mrefu na halali na wao.
Kwenye ujumbe mzito uliovuja kupitia vyombo vya habari nchini Uhispania, viongozi wa Atlético hawakung'ata maneno:"Kila mtu anajua kuwa hii ni klabu ya udanganyifu. Lakini safari hii wamegonga mwamba, wamekutana na klabu isiyoweza kufanyiwa mzaha."
Kisasi cha Kale:
Kumbukumbu ya Griezmann Yaibuliwa Kile kinachofanya mgogoro huu kuwa mbaya zaidi ni historia kati ya timu hizi mbili.
Atlético wametumia fursa hii kukumbushia sakata la miaka ya nyuma la Antoine Griezmann. Wanadai kuwa Barcelona wana tabia ya "kiharamia" ya kuwarubuni wachezaji na familia zao wakati timu pinzani zikiwa katikati ya mashindano muhimu, jambo ambalo wanataja kama ukosefu wa maadili ya kimichezo.
Hatua Inayofuata: Dau la Euro Milioni 500?
Msimamo wa Atlético Madrid kwa sasa umenyooka: hawataki fedha za Barcelona na hawapo tayari kufanya biashara yoyote ya kiungwana.
Vyanzo vya karibu na klabu hiyo vinasisitiza kuwa njia pekee ya Julián Álvarez kuondoka na kwenda Camp Nou ni kama Barcelona wataamua kulipa kipengele chake cha ndani cha mkataba ambacho kinatajwa kufikia Euro milioni 500—kiasi ambacho ni kikubwa kwa hali ya sasa ya kiuchumi ya Barcelona.
Sakata hili la Álvarez sasa linatazamwa kama mtihani mkubwa wa kisheria na kiutawala.
Je, Barcelona watafanikiwa kunasa saini ya Julián Alvarez au watakumbana na rungu la FIFA? Weka comment yako kama we ni mshabika na mfatiliaji wa mpira kwa undani zaidi👇👇

Comments
Post a Comment
Maoni yako ni muhimu kwetu! Unafikiri nini kuhusu mchezo au tetesi hii ya leo? Shusha mchango wako hapa chini. Kumbuka: Lugha ya staha na heshima kwa wadau wote wa soka inazingatiwa.