VIWANJA NANE KUWAKA MOTO: Raundi ya 29 ya NBC Premier League Kupigwa Leo kwa Muda Mmoja.
Msisimko wa Ligi Kuu ya NBC unafikia kilele chake leo Jumamosi ya tarehe 27 Juni, ambapo timu zote 16 zitashuka dimbani kucheza michezo nane ya raundi ya 29 kwa muda mmoja, saa 10:00 jioni. Hatua hii ya Bodi ya Ligi imelenga kuongeza ushindani wa haki na kuzuia mianya ya upangaji wa matokeo, huku presha kubwa ikiwa pande zote mbili; zile zinazowania ubingwa na zinazopambana kushuka daraja.
Macho ya mashabiki wengi yatakuwa jijini Dar es Salaam ambapo Young Africans watakuwa wenyeji wa TRA United kwenye uwanja wa KMC Complex, huku majirani zao Simba SC wakicheza dhidi ya Singida Black Stars kwenye dimba la Meja Jenerali Isamuhyo lililopo Mbweni. Vita nyingine kali itakuwa mkoani Tanga ambapo Azam FC watakuwa wageni wa Coastal Union, mchezo utakaotoa mwelekeo wa nani atakayeshika nafasi za juu za msimamo msimu huu.

Comments
Post a Comment
Maoni yako ni muhimu kwetu! Unafikiri nini kuhusu mchezo au tetesi hii ya leo? Shusha mchango wako hapa chini. Kumbuka: Lugha ya staha na heshima kwa wadau wote wa soka inazingatiwa.