Mashati ndani, Mzee wa kucheka na nyavu: Ni nini sababu ya Yanga sc kumsajili Peter Shalulile kwenye klabu hiyo.

Ule usajili uliokuwa ukisubiliwa kwa hamu na mashabiki wa Yanga SC pamoja na barani Afrika kwa ujumla, Yanga SC imemtambulisha Raia wa Namibia, Peter Shalulile usiku wa kuamkia leo baada ya kuinasa saini ya mchezaji huyo baada ya kuwa mchezaji huru, Utambulisho huu umewashitukiza mashabiki wengi wa soka. 


Peter Shalulile amejiunga na wanajangwani, Yanga SC kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kuachana na miamba wa soka wa kimataifa wa Afrika Kusini,Mamelodi Sundowns. Mzee wa kuchomekea alikuwa huru alipomalizana na timu yake ya zamani Mamelodi na kuwa huru , akashawishika na soka la bongo NBC Premier League, Shalulile mwenye umri wa miaka 32 mwenyi kiwango cha hali ya juu sasa hivi ni mali ya yanga.


Ujio huu kwa timu ya Yanga sc inatarajia kuwa na mwendelezo mzuri wa mashindano ya ndani na ya kimataifa. Peter Shalulile ni mchezaji mwenye hazi ya kimataifa amefanya makubwa kwenye mashindano ya Afrika Kusini na kuisaidia timu yake ya Mamelodi Sundowns kutwaa ubingwa mara kibao na kuwa mfungaji bora wa mda wote wa ligi ya Kusini kwa kufunga magoli zaidi ya 100. 

Maswali yapo kwa mashabiki wengi wa soka kuwa usajili huu mzito wa Yanga sc kwa msimu huu kuna timu yoyote ya ligi kuu kama Simba sc na Azam Fc italeta ushindani wowote au kombe linarudi tena kwa wanajangwani, Yanga sc ?. 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA ALPHONCE MSANGA (MABULA) YA SOKA: Kutoka kwenye maisha ya mtaani hadi kuwa mchezaji bora wa kimataifa

Wachezaji bora kwenye ligi kuu ya NBC Premier League

Wasifu wa Albert Kangwanda Jr: Nyota Mpya wa Kimataifa Anayetamba Ndani ya Kikosi cha Yanga SC

RIPOTI KUTOKA KAMBINI: Uchambuzi wa Kikosi cha Taifa Stars na Silaha Mpya Kuelekea AFCON 2027

Fabrizio Romano Aitambulisha Yanga Duniani, Bodi ya Ligi Yaibeba Simba SC!

Rungu la TPLB: Maafisa wa Singida Black Stars Watandikwa Faini ya Tsh Milioni 20!

Mtanange wa Ligi Kuu ya NBC: Uchambuzi wa Kina wa Mechi za Kukata na Shoka Kesho

Mwelekeo wa Ligi Kuu ya NBC: Rejesho la Aziz Ki, Changamoto ya Majeraha Simba SC na Shinikizo Ndani ya Azam FC

WASIFU KAMILI: Fahamu Nguvu na Udhaifu wa Gaborone United, Wapinzani wa Yanga SC Ligi ya Mabingwa Afrika!

Ratiba Kamili na Utabiri wa Kimbinu wa Michezo ya Ufunguzi Ligi Kuu ya NBC Wikiendi Hii.