KIMEUMANA! YANGA YAPIGWA BAN YA FIFA, SIMBA WAFANYA DUA, IBENGE AKWAMA DAR!
Mambo ni moto huku mtaani! Wakati Yanga wakisherehekea jezi zao mpya za QR Code, FIFA wamewashushia 'zengwe' la kufungiwa kusajili kwa vipindi vitatu kuanzia Agosti 5 kwa kukiuka kanuni za uhamisho. Inasemekana kuna mambo hayajakaa sawa kwenye mikataba, hivyo Wananchi sasa hivi presha inapanda!
Wakati huohuo, kule Msimbazi maandalizi ya kilele cha 'Simba Day' kesho Agosti 8 yamepamba moto, na leo wamefanya dua maalum ya kupata baraka kuelekea msimu mpya. Lakini habari ya kushtusha ni kutoka Azam FC; kocha Ibenge na wachezaji wake wa DR Congo wamekwama Dar na hawajaweza kuungana na timu kule Rwanda kwa ajili ya kambi ya maandalizi. Je, itakuwaje kwenye Ngao ya Jamii? Tupia maoni yako hapa!

Comments
Post a Comment
Maoni yako ni muhimu kwetu! Unafikiri nini kuhusu mchezo au tetesi hii ya leo? Shusha mchango wako hapa chini. Kumbuka: Lugha ya staha na heshima kwa wadau wote wa soka inazingatiwa.