๐ฆ๐๐๐จ๐ ๐ฆ๐๐ ๐๐ ๐ฆ๐ฃ๐ข๐ฅ๐ง๐ฆ ๐๐๐จ๐: ๐ ๐ฎ๐ณ๐ฎ๐ป๐ถ๐ธ๐ถ๐ผ ๐๐ฎ ๐๐ถ๐บ๐ฏ๐ฎ ๐๐ผ๐ธ๐ฎ ๐ญ๐ต๐ฏ๐ฒ ๐บ๐ฝ๐ฎ๐ธ๐ฎ ๐น๐ฒ๐ผ
Simba Sports Club ni timu ya Tanzania iliyoanzishwa mwaka 1936, badaa ya viongozi baadhi kugawanyika kutoka Yanga sc na wengini kuanzisha hii timu. Simba SC ilipoanzishwa ilijulikana kwa jina la kwanza la Queens, badae ikabadilishwa jina na kuitwa Eagles, kisha ikaitwa Sunderland, na tangu mwaka 1971 ilijulikana kwa jina la SIMBA SPORTS CLUB.
Al Ahly SC (Misri) Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) Espรฉrance de Tunis (Tunisia) RS Berkane (Morocco) Pyramids FC (Misri) Simba SC (Tanzania) Zamalek SC (Misri)
Simba Sc ni timu maarufu na yenye mafanikio makubwa kwenye soka nchini Tanzania na Afrika Mashariki na Kati kwa ujumla. Makao makuu ya Simba Sc yapo mtaa wa Msimbazi- Kariakoo, Dar Es Salaam, inchini Tanzania.
Uongozi na Umiliki wa Simba SC
1.Uwekezaji; Simba SC inaendeshwa na utaratibu wa hisa na muwekezaji mkuu na MO Dewji . Uwekezaji wa Mohammed Dewji (MO Dewji) hisa yake anachukua asilimia 49% na wanachama wengine wanachukua 51%.
2.Mwenyekiti; Simba SC inaongozwa na mwenyekiti Murtaza Mangungu.
Mafanikio ya Simba SC
•Ligi Kuu Tanzania; imetwaa ubingwa mara 29.
•Ligi muungano; inakadiliwa imetwaa mara 6 na kuendelea
•FA/CRDB BANK Federation Cup; inakadiliwa mara 6 na kuendelea
•Ngao ya jamii; imetwaa mara 10
•Kagame cup; inetwaa mara 6
•Mapinduzi Cup; imetwaa mara 3
•CAF Champions League ; imefika robo mara 4 na nusu mara 1 mwaka 1974.
•CAF Confederation Cup ; imefika fainali mara 2 na robo mara 1
•Goli bora Afrika; simba ilitwaa goli bora Afrika nzima kupitia mchezaji wao wa zamani Pape Ousmane Sakho.
Malengo ya Simba Sc msimu huu
•Kutwaa ubingwa wa kila mashindano yote anayoshiriki.
•Kuwa na wachezaji bora wenye ngazi ya Kimataifa
• Kuendeleze viwango vya wachezaji na kuwauza
Sherehe za Simba SC/ Simba Day
Kila inapofika mwezi wa Nane(Agosti), Simba SC huandaa tamasha la utambulisho wa wachezaji, benchi la ufundi na jezi.
Ranking ya Simba Sc
Kwa ngazi ya CAF Champions League, simba imeshika nafasi ya sita 6

Comments
Post a Comment
Maoni yako ni muhimu kwetu! Unafikiri nini kuhusu mchezo au tetesi hii ya leo? Shusha mchango wako hapa chini. Kumbuka: Lugha ya staha na heshima kwa wadau wote wa soka inazingatiwa.