KIMEUMANA! MAGETI YASHAFUNGULIWA UWANJA WA UHURU, NYOMI YA SIMBA DAY NI YA HISTORIA!
Mambo ni moto asubuhi hii ya leo Agosti 8, 2026! Yale maadhimisho ya kihistoria ya Miaka 90 ya klabu ya Simba SC (tangu 1936) yameanza rasmi, na mageti ya Uwanja wa Uhuru yameshafunguliwa tangu saa 4 asubuhi hii.
Mitaa yote ya Dar es Salaam sasa hivi imeshakuwa nyekundu na nyeupe. Mashabiki wanamiminika kwa kasi ya hatari huku kila mmoja akitaka kushuhudia kilele cha tamasha hili la kibabe. Leo ndio ile siku ambayo Ahmed Ally aliahidi kuingia kwa ungo wa mchana kweupe, na vikosi vipya vinaletwa machoni mwa Wanasimba! Kama upo nyumbani, weka bando lako karibu kwa sababu kurasa hii itakuletea kila kinachojiri sekunde baada ya sekunde. Mnyama ana jambo lake leo!
Wewe utatokea pande zipi leo kushuhudia shughuli hii? Tupie maoni yako hapa chini!"

Comments
Post a Comment
Maoni yako ni muhimu kwetu! Unafikiri nini kuhusu mchezo au tetesi hii ya leo? Shusha mchango wako hapa chini. Kumbuka: Lugha ya staha na heshima kwa wadau wote wa soka inazingatiwa.